Eti wanaume wafupi ni waume bora?





Wanaume ambao ni wafupi kwa kimo mara nyingi wanasifika kuwa waume bora kuliko wanaume warefu.
Pia inaarifiwa huwa na busara zaidi kufidia kimo chao, amekiri Adam Gopnik, mwanamme mmoja wenye umbo dogo.
Wiki kadhaa zilizopita, wana soshologia wawili kutoka Chuo Kikuu cha New York, walichapisha waraka mrefu ulioangalizia maisha ya watu wafupi.
Utafiti wao ulizua mjadala mkali kutoka kwa kile kinachoweza kusemekana kuwa jamii ya wanaume wenye kimo kifupi.
Waandishi wa waraka huo wa maswala ya kijamii unaashiria kwamba wanaume wenye haiba ya kuvutia mara nyingi hupendelewa katika maisha yao hivyo wanaripotiwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na zaidi ya mpenzi mmoja.
Hata hivyo, hitimisho la waraka huo, pindi mtu anapoupitia, unashangaza. Ni kwamba, watu wafupi wana ndoa za kudumu zaidi.
Wanafanya hayo, katika mazingira magumu wakiwa katika umri tofauti na kipato tofauti, na wanayafanya hayo wakiwa na wanawake wafupi ambao wanawaoa, na wakati mwengine na hata wanawake warefu wanaokutana nao.
Wanaume wafupi wanaoa kuchelewa, lakini pindi wanapooa, wanadumu katika ndoa kwa muda mrefu, na kwa kiwango cha sayansi ya kijamii, angalau wanakuwa na furaha.
Kuna sababu zinazoonyesha kwa nini wanaume wafupi wanadumu kwenye ndoa.
Nazo ni, wanaume wafupi wanaonyesha kukata tamaa. Wanaume wafupi wanaishi katika ulimwengu wa wanaume warefu na wanajua kila fursa inayopatikana, ni bora kuidhibiti.
Hali ya kukata tamaa ndio inayowafanya wanaume wafupi kuwa wanaume bora kwa wake zao. Watafiti hao pia walisema kuwa wanaume wafupi hukimbilia kufanya kila kitu kuwafurahisha wapendwa wao wakati wanume warefu hilo halliwajalishi.