MASHINDANO YA UKAMUAJI MAZIWA YAZUA MASWALI

Photo: MASHINDANO YA UKAMUAJI MAZIWA YAZUA MASWALI
Mashindano ya kukamua maziwa mwaka huu yameleta wasiwasi wa baadhi ya washiriki kutumia dawa za kuongeza nguvu. Michuano ya dunia iliyofanyika nchini Italy, imeshuhudia bingwa akikamua lita 8.7 katika kipindi cha dakika mbili. Mshindi alikuwa Gianmario Ghirardi na ng'ombe wake Mirka. Hata hivyo washindi watatu wa juu mwaka huu wamekabiliwa na tuhuma za matumizi ya dawa za kuongeza nguvu baada ya washindi hao wote kukamua maziwa zaidi ya lita saba katika kipindi cha dakika mbili. Kwa mujibu wa tovuti ya i100, bingwa wa mwaka 2013 Maurizio Paschetta amesema: "Kwa mashindano makiubwa kama haya, ungetegemea vipimo vya matumizi ya dawa kufanyika kwa ng'ombe na hata wakamuaji, ili kuwepo na hakikisho la  uwazi katika nafasi za juu."
Hata hivyo msaidizi wa rais wa shirikisho lililoandaa michuano hiyo amesema; "Tuliwapima ngombe wote kwa muda wa saa moja, halafu pia kuna majaji wanane."