MWANASHERIA Mkuu wa Zanzibar, Othman Masoud Othman, jana alinusurika kupigwa na wajumbe wenzake wa Bunge Maalumu la Katiba baada ya mwanasheria huyo kupiga kura ya wazi ya “hapana,” kukataa rasimu ya Katiba inayopendekezwa na Bunge hilo.
Awali, Othman alikuwa amesusia Bunge hilo na kujiuzulu katika kamati ya uandishi iliyoandaa rasimu hiyo, akidai kwamba hoja 17 za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) zimepuuzwa katika katiba mpya.
Ads by HD01-V2.1V27.09×Jana asubuhi, mwanasheria huyo aliingia ghafla ukumbini, muda mfupi baada ya Bunge kuanza huku baadhi wajumbe ambao hawakuwepo wakati wa kupiga kura, wakiwa wamemaliza kufanya hivyo, lakini wakati Mwenyekiti wa Bunge, Samuel Sitta, akimalizia matangazo ili kuahirisha Bunge. Ndipo alipotaarifiwa kuwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar alikuwa amefika, apewe nafasi ya kupiga kura.
Othman alisimama taratibu, kwa kusitasita mithili ya mtu aliyelazimishwa, akasema, “napiga kura ya wazi, na vifungu ambavyo sivikubali ni ibara ya 2, 9, 70, 71,72,73,74, 75, 128,129,158,159,160,161,243 hadi
251 na nyongeza ya kwanza, vingine vilivyosalia navikubali.”
251 na nyongeza ya kwanza, vingine vilivyosalia navikubali.”
Vifungu alivyokataa vinahusu mamlaka ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (2), ukuu wa katiba (9), muundo wa muungano (70), utekelezaji wa shughuli za mamlaka ya nchi (71), mamlaka ya serikali ya jamhuri ya muungano (72) na mamlaka ya serikali ya Mapinduzi Zanzibar yasiyo ya
muungano (73).
muungano (73).
Uhusiano kati ya serikali ya jamhuri ya muungano na serikali ya Mapinduzi Zanzibar (74), wajibu wa viongozi wakuu kulinda muungano (75), madaraka ya kutunga sheria (128), utaratibu wa kubadilisha katiba (129), SMZ na mamlaka yake (158), Rais wa Zanzibar na mamlaka yake (159), Baraza la Mapinduzi la Zanzibar na kazi zake.
Baraza la Wawakilishi la Zanzibar (161) na kuanzia ibara ya 243 hadi 25, inahusu Mfuko Mkuu wa Hazina na Fedha za Jamhuri ya Muungano wakati nyongeza ya kwanza ni kuhusu mambo 16 ya muungano.
Baada ya Othman kupiga kura hiyo, Bunge lilionekana kutaharuki hususani wajumbe kutoka Zanzibar, na muda mfupi baadaye alisimama Yahaya Kasimu Issa na kuomba aruhusiwe aseme kidogo.
“AG amepiga kura wakati kwenye mjadala hakuwepo… na si kwamba alikuwa anaumwa bali kwa kejeli yake ya kuonesha kwamba amesoma.
“Tulitegemea awepo hapa tangu mwanzo lakini yeye akatoroka…hivi mwanasheria kama huyu ana maslahi gani kwa Wazanzibari? Yaani Rais amemteua awe msaidizi wake wa kazi lakini yeye ametoroka…hivi unaweza kutuambia tuna maslahi gani na mtu kama huyu?” Alihoji huku akishangiliwa.
Wajumbe wenzake wa Zanzibar walianza kupiga makofi na kumzomea mwanasheria huyo wakimwita “kamanda aliyekimbia vita, msaliti, UKAWA, hafai aondoke,” na kejeli nyingine, lakini yeye alikuwa mtulivu tu kwenye kiti chake.
Baada ya kuona vurugu hizo, Sitta aliinuka na kutangaza kufunga mjadala huo huku akiwataka wajumbe waache kumwandama mwanasheria huyo kwa kuwa kikatiba na kisheria, anao uhuru wa kuamua anavyoona inafaa kwani mle ndani hajaingia kwa wadhifa wake bali amepiga kura kama mjumbe.
Kauli hiyo ya Sitta, haikufua dafu kwani baada ya Bunge kuahirishwa,Wazanzibari wengi waliendelea kumzomea huku wakiinuka kwenye viti na kuanza kumfuata wakitaka kumpiga.
Baadhi ya viongozi wakuu wa Zanzibar, wakiongozwa na Makamu wa Pili wa Rais, Balozi Seif Idd waliingilia kati na kisha askari wa Bunge walizingira eneo hilo na kumwondoa wakimpitisha mlango wa viongozi wakuu.
Hata huku nje, Wazanzibari wengi walionekana kuwa na ghadhabu, wakimsubiri kumshambulia, huku wakihoji ni kwanini alikuja wakati alisusia vikao wakiwa kwenye kamati.
Hata hivyo, baadhi ya wajumbe wa Bara walisema walichukizwa na kitendo cha Wazanzibari kutokuwa wavumilivu wa uhuru wa mawazo ya mtu.
Baada ya hali kuwa shwari na wajumbe wengi kuwa wametawanyika, askari wa kikosi cha kutuliza ghasia (FFU) wakiwa na wapambe wa Bunge walisogea nyuma ya ukumbi wa Bunge kwenye mlango anaotumia Waziri Mkuu na kulizunguka gari la Spika wa Zanzibar, Pandu Ameir Kificho.
Muda mfupi baadaye viongozi wakuu wa Zanzibar takribani kumi walitoka nje wakiongozana na mwanasheria mkuu huyo, ambaye alipanda kwenye gari moja na Kificho kisha wakaondoka eneo la Bunge huku wakisindikizwa na maofisa usalama.
Ndani ya viwanja vya Bunge, Wazanzibari walionekana kukusanyika vikundi vikundi wakijadili tukio hilo huku wengine wakiwa wamekaa pekee yao, wakionekana kunyong’onyea.
Sitta na kura za UKAWA
Maajabu ya Bunge la Katiba, hayakuishia hapo, bali hata Sitta aligeuka ahadi yake ya wiki iliyopita ya kwamba kura za wajumbe wote wa kundi la Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) waliosusia ni za hapana, safari hii akitamba kuwa wajumbe wawili wa UKAWA wamepiga kura ya ndiyo wakiwa nje ya Bunge.
Hata hivyo, hatua hiyo huenda ikaibua mgongano wa kisheria kwani tayari baadhi ya wajumbe wameanza kuhoji inawezekanaje mjumbe ambaye hakuwahi kushiriki kujadili katiba kwa makusudi aruhusiwe kupiga kura tena akiwa nje ya Bunge.
Akizungumzia taarifa za baadhi ya wajumbe kulalamika kutishwa kiasi cha wengine kuruhusiwa kuondoka, Sitta bila kutaja majina aliliambia Bunge.
“Baada ya tangazo langu kwamba wale wote waliyoko nje
watapiga kura, wajumbe wawili ambao walikuwa kwenye ule mgomo wa kile kiukundi cha UKAWA wameisoma katiba inayopendekezwa wakaona ni kitu cha kizalendo kuipigia kura”.
watapiga kura, wajumbe wawili ambao walikuwa kwenye ule mgomo wa kile kiukundi cha UKAWA wameisoma katiba inayopendekezwa wakaona ni kitu cha kizalendo kuipigia kura”.
Sitta alisema kuwa wajumbe hao kutoka Zanzibar, mmoja wao yuko radhi kufukuzwa uanachama wa chama chake baada ya kupiga kura hiyo na kutamba kwamba Mwenyezi Mungu akitaka jambo liwe, litakuwa.
Kuhusu vitisho kwa wajumbe, alisema kuwa baadhi ya watu wasiotaka mchakato huo uende vizuri wamediriki kuwafungia wajumbe wasipige kura na ilibidi Bunge litumie vyombo vya usalama kumkomboa mjumbe aliyefungiwa.
“Tukio la pili kuna wajumbe wawili walifika kwa Katibu wa Bunge na kuonesha ujumbe wa vitisho…waliogopa sana na tukawaruhusu waondoke, wametishwa sana kwamba wasiendelee kubaki hapa…vitisho hivyo nayo ni jinai.
“Tazama jana mjumbe Mwanaidi aliniandikia kuwa jina lake lilirukwa wakati tunapiga kura, lakini Mwenyekiti wake wa Chama cha NRA, alikuwa ameniandikia kwamba mjumbe yule alipiga kura ya hapana akiwa hajaelewa, kwamba pengine kuwe na mashauriano, nikamjibu kuwa atapiga
baada ya mashauriano na kamati,” alisema Sitta.
baada ya mashauriano na kamati,” alisema Sitta.