Mbowe mikononi mwa polisi......JOPO la Mawakili wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), na wanachama wa chama hicho, leo wamepanga kumsindikiza mwenyekiti wao Freeman Mbowe aliyeitwa Makao Makuu ya Polisi kwa ajili ya mahojiano.
Akizungumza na Waandishi wa Habari katika Makao Makuu ya CHADEMA yaliyopo Kinondoni Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Willibrod Slaa, alisema barua ya kumwita Mbowe polisi waliipata juzi wakiwa katika kikao cha Kamati Kuu.
“Tukiwa tunaendelea na kikao cha Kamati Kuu ya chama … tulipata barua toka Jeshi la Polisi iliyoandikwa na Naibu Kamishna Hezron Gimbi, ikimtaka mwenyekiti wetu aende kwa mahojiano…bahati nzuri chama chetu kina wanasheria wengi, hivyo tulilijadili na kukubaliana kuwa aende kuwasikiliza,” alisema Dk. Slaa.
“Nawataka vijana wangu wa Bavicha, wanawake na watoto kupiga kelele kuhusu hili wanalotaka kulifanya polisi…nasisitiza kwamba, tunahitaji na tutakuwa na umoja, amani, mshikamano iwapo polisi watafanya kazi kwa vyombo vyote kwa mujibu wa sheria,” alisema.
Septemba 14 mwaka huu, akiwahutubia wanachama wa chama hicho katika mkutano mkuu, Mbowe alisema kwa kukubaliana na viongozi wenzake wa UKAWA, watatangaza maandamano na mmigomo bila kikomo nchi nzima kushinikiza kusitishwa kwa Bunge la Katiba, waliloliita la kifisadi linaloendelea mjini Dodoma.
Mbowe, alisema umefika wakati sasa wa kuacha kukaa na kuzungumza kwa kuwa kinachoendelea Dodoma ni wizi na ukatili wa hali ya juu kwa wananchi wanyonge ambao ndio walipa kodi.
“Samahani…maneno yangu ni makali na wala hapa sifanyi uchochezi…kinachoendelea Dodoma ni ufisadi na wizi, tumekaa Kinana, tumekaa na Mangula, tumekaa na Rais Kikwete tumekubaliana bunge lisitishwe, lakini wanamwacha Sitta afanye anachotaka kama utafikiri ndiye Rais…
“Anachakachua rasimu, anabadili kanuni, anavunja sheria anakusanya maoni utafikiri yeye ni Warioba…hiki hakivumiliki, naomba mkutano huu utoke na tamko,” alisema Mbowe na kushangiliwa na wajumbe kama alama ya kuafiki.
Hata hivyo, jana akizungumzia kuhusu kauli ya Mbowe ya Septemba 14 mwaka huu, Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA, Tundu Lissu, alisema hakuna kosa lolote alilolifanya Mbowe kwa kuwa alikuwa akihutubia mkutano wa chama chao ambao ulikuwa upo kihalali.
Dk. Slaa, alisema ingawa hawajui jambo lililofanya Jeshi la Polisi limwite Mbowe kwa ajili ya mahojiano, wanahisi kwamba yawezekana wanataka kuifanyia kazi kauli ya Waziri wa Sheria na Katiba, Dk. Asha Rose- Migiro, kwamba mjadala wa kusitisha bunge umefungwa rasmi hapo jana licha ya kuwepo kwa madai kuwa bunge hilo halina uhalali wa kisiasa.
Alisema kwa kuwa Jeshi la Polisi limekuwa likiongozwa na kauli za viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), na serikali bila kuangalia sheria inasema nini, hivyo kutaka kumzima Mbowe baada ya kutoa kauli ya kuwataka wanachama na watanzania kwa jumla kuandamana kwa ajili bunge la katiba lisitishwe.
Dk. Slaa, alisema hakuna kesi pamoja kwamba Jeshi la Polisi litakwenda kumhoji Mbowe, suala la maandamano yenye kuonyesha chuki, hasira kuhusu unafiki na wizi wa fedha za wananchi unaoendelea huko Dodoma halitasimama.
“Tunaendelea kupokea taarifa za viongozi wa ngazi za Kata, Majimbo na Mikoa namna watakavyofanya maandamano yao…ili tukishamaliza uratibu wa pamoja na washirika wenzetu wa UKAWA, tutaeleza siku rasmi ya kuanza,” alisema.
Katibu Mkuu huyo, alisema CHADEMA haitakubali kuona mwenyekiti wao anachukuliwa sheria yoyote hiyo kesho, kwa kuwa hakuwa na kosa lolote la kutoa tamko kwa wanachama wake ambao waliridhia kama maazimio ya pamoja.“Niliposoma barua toka polisi ikimtaka mwenyekiti wangu aende kwa mahojiano ambayo hayaelezi kosa…nilitoa ushauri wa kisheria kuwa aipuuze kwa kuwa haikujitosheleza, lakini baada ya mashauriano na wajumbe wa Kamati Kuu tukaona aende tu,” alisema Lissu.
Lissu, alisema kwa kuwa Jeshi la Polisi limekuwa na tabia ya uonevu miaka yote kwa raia wake katika masuala ya haki, wamejipanga vema kisheria kwa ajili ya utetezi wa amri ya polisi ya kutaka kumhoji mwenyekiti wao leo.
Naye akijibu swali la mwandishi aliyetaka kujua idadi kamili ya jopo litakaloongozana na Mbowe, Naibu Katibu Mkuu Bara, John Mnyika, alisema kiongozi huyo ataambatana na mawakili wote wanaotetea chama hicho na wanachama, akiwamo Mwanasheria Mkuu wao Lissu.
Mawakili wengine watakaoambatana na Mbowe, ni mawakili nguli na viongozi wa chama hicho, Profesa Abdalah Safari, Mabere Marando, Peter Kibatara, Halima Mdee, Nyaronyo Kicheere, John Mallya, Jonathan Mdeme na wengine.
Wakati huo huo, Dk. Slaa alisema mkutano mkuu wa chama hicho uliazimia kwa kukubali ushirikiano uliyopo kati yao na vyama vya upinzani vilivyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA).Hivyo, alisema katika kukubali ushirikiano huo, wamekubali kushirikiana katika suala la uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika Desemba 14 mwaka huu kwa kuunda timu ya maandalizi kwa kila chama kwa ajili ya kuukabili.
“Kamati Kuu imeunda ‘task force’ ya kuona namna ya kushirikiana katika uchaguzi huo, inayowajumlisha Profesa Safari, John Mnyika, John Mrema, Benson Kigaila na Tundu Lissu, ambayo imeanza vikao vyake leo hii,” alisema Dk. Slaa.
Katika hatua nyingine, Kamishna wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi, Paulo Chagonja, alisema jana kwamba, wameanza kupokea taarifa za CHADEMA ikitaka kufanya maandamano katika maeneo mbalimbali hapa nchini kuanzia leo, lakini maandamano hayo yanaenda kinyume na sheria na hayataruhusiwa.
Nao Danson Kaijage na Hamida Ramadhani,wanaripotikutoka Dodoma kuwa, Jeshi la Polisi mkoani humo, limetangaza kuzuia maandamano yanayoratibiwa na wanachama wa CHADEMA mjini hapa.
Akitangaza kuzuia maandamano hayo, Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Emmanuel Lukuna, alisema jeshi hilo limezuia maandamano hayo kwa sababu yanapingana na sheria ya kuwepo kwa Bunge Maalum la Katiba na kwa kuruhusu maandamano ni kuvunja sheria.
Alisema licha ya viongozi wa CHADEMA Mkoa kupeleka barua ya kutoa taarifa ya kufanyika kwa maandamano ya amani ambayo yanatarajiwa kufanyika leo, lakini jeshi la polisi limezuia kutokana na kutokukidhi vigezo.Lukuna, alisema kuwa wamejipanga kuhakikisha wanazuia maandamano hayo kutokana na kuwa, yanalenga kufanya vurugu ya kutaka kuzuia Bunge Maalum la Katiba.
Mbali na hilo, alisema kuwa maombi mengine ambayo yametoka wilayani hayakukidi vigezo kwani yamecheleweshwa kufika.
Hata hivyo, alisema kuwa viongozi wa CHADEMA Mkoa wamepinga kuzuiliwa kwa maandamano na kuonesha msimamo wao wa kufanyika leo.