Msaada wa kibindamu umeanza kutolewa kwa maelfu ya waathiriwa wa mapigano waliosalia katika mji wa Kobane nchini Syria ambao wanatarajiwa kuanza kuhamishwa.
Wapiganaji wa kundi la IS waliuteka mji huo Jumatatu na kuzua hofu ya kutokea kwa mauaji ya halaiki.
Umati mkubwa wa watu tayari umeondoka mjini humo na kuikimbilia nchi jirani bya Uturuki. Magari ya kuwabeba wagonjwa mahututi yameonekana yakiwabeba maelfu ya watu waliojeruhiwa katika vita vinavyoendelea kati ya wapiganaji wa IS na muungano wa majeshi ya kivita.
Awali afisa wa Kikurdi ndani ya mji huo Asya Abdullah, alionywa kuwa iwapo vikosi vinavyoongozwa na Marekani havitokoma kufanya mashambulio huenda kukatokea mauaji ya halaiki.
Mashambulizi ya angani yameripotiwa kusikika katika mji wa Kobane asubuhi ya leo baada ya ndege za kivita za Marekani kusikika zikiruka angani kwa saa kadhaa.
Usiku kucha makabiliano yalitokea kati ya polisi na vikundi vya watu wa jamii ya wakurdi, katika miji kadhaa ya Uturuki. Wanalalamika kwamba, majeshi ya Utruruki hayajaingilia mzozoro huo hadi sasa.
Vita hivyo vimeripotiwa kuenea hadi katika eneo la Kusini mwa Kobane katika mpaka wa Uturuki. Mpaigano yameripotiwa kuchacha hasa baada ya wapiganaji wa IS kuteka mitaa mingine mitatu mjini Kobane.
Zaidi ya watu 160,000 wengi wao wakurdi wametoroka mji wa Kobane hici karibuni.
Ikiwa wapiganaji wa IS wauateka mji huo wote basi watakuwa wanadhibiti sehemu kubwa ya mpaka wa Syria na Uturuki.