Watuhumiwa hao wameachiwa huru na Mahakama ya Kwale baada ya kukaa jela kwa zaidi ya wiki mbili kwa kosa la kufanya mkutano kinyume cha sheria.
Mwamnuadzi na wenzake walikamatwa oktoba15 huko Komabi ambapo walifunguliwa mashtaka kwa kosa la kufanya mkutano kinyume cha sheria ambapo washtakiwa walipinga kutenda kosa hilo.
Baada ya kusomewa mashtaka katika mahakama ya Kwale, washtakiwa walipelekwa gereza la shimo la Tewa, Novemba 3.
Kesi hiyo itasomwa tena Januari 12 mwaka 2015.